Matthew 4:18-19

18 aIsa alipokuwa anatembea kando ya Bahari ya Galilaya, aliwaona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea ndugu yake. Walikuwa wakizitupa nyavu zao baharini kwa kuwa wao walikuwa wavuvi. 19 bIsa akawaambia, “Njooni, nifuateni nami nitawafanya mwe wavuvi wa watu.”
Copyright information for SwhKC